Maombi ya Manchester United(Stolen)
Baba tunakuja mbele zako siku hii ya
leo. Baba tunakutambua, wewe ndio
mwenye uwezo, mwenye nguvu na
mwenye hekima isiyo na mipaka.
Baba sisi ni watenda dhambi na
tunajinyenyekea na kusujudu mbele
zako leo hii kukuomba mambo
yafuatayo.
Kwanza Baba tusamehe kwa kushabiki
Red Devils miaka hizi zote, hatukujua na
tunajipiga moyo konde kwa imani kuu
utatusamehe kwa sababu wewe
umejawa na rehema tele.
Pili tunakuomba Baba umtume malaika
wako wa uponyaji, malaika Raphaeli
atunyunyuzie maji ya painkillers ili
maumivu tuliyoletewa na Moyes yaishe.
Tatu Baba tunaomba utume radi tatu
kule Trafford. Radi ya kwanza imtandike
David Moyes hadi apoteze fahamu ili
tupate kocha mpya.
Radi ya pili Baba imtandike Ashley
Young na kumrusha kwenye maji ili
awe samaki asirudi uwanjani tena.
Radi ya tatu umtumie David Moyes tena
ili ihakikishe amepoteza fahamu vizuri
Ombi la nne Baba tunaomba mkono
wako unyunyizie Manchester City zile
baraka ambazo zilikua zetu ili hicho
kikombe kisiende kwa wale washerati
ya Merseyside au wale ma Pharisayo wa
North London ambao walimsulubisha
mwanao.
Ombi la tano Baba tunakusihi uwatishie
Gundogan, Reus na Juan Mata na
vitisho vya moto ya jehanamu ili watie
sahihi katika kitabu cha Old Trafford.
La sita Baba tunakuomba uwafanye
watu wote wa London wapoteze sauti
zao ili tupate amani na ladha yetu ya
maisha irudi.
La saba Baba tunakuomba uingilie kati
between sasa na May utuokoe kutokana
na janga la relegation, tunakuomba
utume malaika wako watubebe kutoka
katikati ya meza hadi nambari ya
4….ama watubebe hadi nambari ya 5
tutambea sisi wenyewe hadi top 4.
La nane Baba tuma uponyaji kwa miguu
ya Robin Van Persie na mood swings za
Wayne Rooney. Na iwapo Baba itatokea
situation ambapo Rooney atahama
tunakusihi Baba umnyang’anye nywele
tena.
La Tisa Baba ni asante kubwa kwa
kutuondolea Anderson, twajua wewe
hupata maombi mengi sana lakini
twakuomba kama itawezekana
uwafanye waliochukua Anderson
warudi na kuwabeba Evra, Rio
Ferdinand na kwa mara nyingine tena
David Moyes.
La kumi na la mwisho Baba ni ku
kukumbusha kuhusu lile ombi la Tatu,
tafadhali Baba usisahau kutuma hizo
radi.
Ni hayo tu baba, kwa niaba ya majeruhi
wenzangu tunasema asante kwa hivyo
vikombe vyote na usitusahau msimu
ujao. Sisi bado ni watu wako Baba.
Asante.