Swali langu kwa @Mrembo aka @Pretty ni hili?
Je sisi ambao hatukuweza hata kununua vitabu vya fasihi,na kwa hivyo hatukuisoma,tunaweza kuwa twatumia kiasi gani cha akili zetu?
Wajinga kama mimi twawezaje kuepuka kuwa watumwa wa wengine. Lakini nakwambia ni heri kuwa mtumwa kuliko kuwa mwombaji. Na ni kama ulivyosema hapo awali, wanaume wengine ni lazima wawe watumwa. Lakini utumwa ni wa aina nyingi - na ikiwa wataka bwanako asiajiriwe kazi ili awe mtumwa wako huko nyumbani,basi namhurumia! Utakachomuomba Mungu atakupa. Endelea kuomba na hatimaye utakipata utakacho.
Yaonekana wafanya kazi katika Shirika lisilo la Kiserikali. Huko ndiko wapata pesa zako? Pesa aina hiyo ni ya kuomba na uombaji nauchukia kabisa. Ni kheri kuwa mtumwa kuliko kuomba. Ama pengine wapeleka pesa za babako huko shirikani?
Mimi na Mke wangu tu watumwa,na twamshukuru Mungu sana kwa kutupa fursa ya kuweza kuwatumikia Wakenya kwa utumwa wetu.
Je waalimu wako huko ulikosomea si walikuwa watumwa pia? Bila wao pengine hungeweza kusema hayo unayojaribu kutuambia.
@ Mrembo - Akili nyingi huondoa maarifa!
All beginnings are difficult ..... ..... everything has an end,only a sausage has two.
Taunet Neelel ..... New Beginning .....