Familia ya Joshua Waiganjo, mshukiwa
anayezuiliwa na polisi kwa kudai kuwa naibu PPO mkoani Rift Valley, imedai kwamba mwanao aliajiriwa na Kamishna wa polisi kuwa polisi wa akiba na baadaye kupandishwa cheo kwa haraka. Babake mshukiwa huyo Ibrahim Waiganjo ambaye ni afisa mustaafu wa polisi na sasa ni mhubiri amesema kwamba mwanaye amekuwa akiihudumia idara ya polisi
kwenye wadhifa wa polisi wa akiba kwa muda.
Amesema aliachishwa kazi wakati wa muhula
wa Kamishna Hussein Ali lakini alipokuja
Mathew Iteere, alimwajiri tena kwenye
huduma iyo hiyo ya polisi wa akiba. Amesema
ni wakati huo ndipo alipandishwa cheo kufikia
naibu mkuu wa polisi mkoani. Waiganjo
amesema hayo kwenye kikao na wanahabari
nyumbani kwake Njoro ambapo pia ametoa
picha zinazoonyesha baadhi ya wakuu wa
polisi wakiwa na mwanaye
http://www.standardmedia...%20'PPO'%20yadai Receive with simplicity everything that happens to you.” ― Rashi