sihingwa wrote:Ninayo uchungu mwingi sana nikimjibu bi/bw Chuse...Shida ya wakenya ni moja tu - ufisadi. Shida ya ndugu zetu wabongo ambayo inawatafuna ni rushwa,kukosa uzalendo,uvivu wa kufikiri na uzembe.
Tatizo hiyo mentality ya watanzania wavivu, wazembe ndio wanayokuja nayo waK kwetu, wakati hayo mawazo yamepitwa na wakati. Watz sio wale mnaowajua kwamba ni wazembe hiki ni kizazi kipya, tuko ngangari. Ukija Tz na hayo mawazo ya uzembe hakuna mtu atakukaribisha kwake. Tunaomba kwa mje taratibu mfanye kazi yenu iliyowaleta na mwende na siyo kutufuata fuata eti wazembe.
WaK walikuwa wanakuja kwetu kufanya kazi halafu wanatulazimisha tuandike kila tunachofanya kwa siku hata ukienda msalani lazima uandike. Sasa sijui mambo ya msalani yatamsaidiaje kwenye kazi yake. Dar sasa karibu nusu ya watu wake ni waK, ukienda Nrb watu wanavaa masuti mpaka unawaogopa lakini kile kinyumba anatoka kwetu wanalala kuku.
Sisi tuko sawa tu maisha yanasonga mbele, SIKU HAZIGANDI hata mkisema.