This must be some regular wazuan sitting behind his comp and laughing so hard at the replies we are giving him. I doubt the guy is Tanzanian!
Lakini nikiweka shuku yangu kando(giving the benefit of doubt), nashangazwa pakubwa na kiwango cha maendeleo katika nchi za Afrika Mashariki ya awali.
Kutoka nikiwa mchanga nilifunzwa katika somo la jiografia kuwa Tanzania ina madini ya Diamond ambayo mwachimba kule Shinyanga katika wilaya ya Mwadui. Baadaye, niliskia kuwa pia mna madini ya Tanzanite na dhahabu na mchanganyiko wa madini mengine mengi.
Waganda nao wana copper huko Kilembe na pia kawi ya kutosha kutoka mto Nile! Juzi wamepata mafuta katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo.
Isitoshe, asili mia kubwa ya ardhi nchini Kenya haiwezi tumika kwa kukuza chakula kwani ni kame na yaweza kaa miaka mingi kabla wenyeji wapate kuvuna chochote.
Vipi basi ikawa Kenya, ambayo madini yake hayatajiki kwa kuwa ni ya dhamani ndogo ikawa na uchumi ulioimarika zaidi? Kwa nini Tanzania, ambayo haina ufisadi wa kiwango kama cha Kenya haimo katika nchi ambazo zimestawi zaidi Afrika?
Tanzania haijakuwa na misukosuko kama ilivyo Kenya na Uganda(tangu wakati mlipondanganywa na Kinjeketile kuwa risasi za Wajerumani zitageuka kuwa maji

).
Ikiwa tuko nyuma yenu kimaendeleo, si mturuhusu basi tufanye kazi na biashara humo Tanzania bila vigezo mtuwekeavyo sasa hivi? Serikali yenu ndiyo inayopinga utengamano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki!
Hata hivyo, ningependa sana kuoa kipusa mtanzania
Kiswahili kyangu kimeishia hapo