Kwanza kabisa ningependa kuchukua fursa hii kumpongeza mwanzilishi wa uzi huu na wote waliochangia mjadala huu kwa lugha sanifu ya taifa HONGERA!
Pili nina bashasha kem kem kwa kuona kwamba kweli wazua kuna ukwasi wa lugha lakini pia nasikitika kua babu guka na wengine walioanguka mitihani ya lugha ya taifa kidogo watakua "wageni" uzi huu unapoendelea kurefuka.
Lakini mbali na haya, imekua ni nadra sana kwangu kupata uzi ulio na manufaa katika kuendeleza fikra na mawazo ya wana wazua.
Naomba kua kupata nyuzi kama hizi humu wazua iwe kitu cha kawaida....
Mwisho naomba kumpa hongera bwana intelligensia kwa kiswahili chake sanifu.
Ijumma njema... naomba ndugu zetu wa phombe wasishiriki kupindukia.
Asanta.